• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la serikali ya Yemen lawaua waasi 80 wa kundi la Houthi

    (GMT+08:00) 2019-04-07 17:26:43

    Jeshi la serikali ya Yemen jana lilitangaza kuwa operesheni ya kijeshi iliyoendelea katika saa 24 iliyopita, jeshi la serikali lilipambana vikali na kundi la Houthi mkoani al-Dhalea, kusini mwa Yemen, ambapo waasi wakiwemo makamanda wasiopungua 80 wameuawa, na wengine wengi kujeruhiwa.

    Kulingana na taarifa za wakazi wa al-Dhalea makumi ya askari wa jeshi la serikali waliuawa au kujeruhiwa kwenye mapambano hayo, hata hivyo kundi la Houthi halijajibu juu ya taarifa hizo.

    Mkoa wa al-Dhalea ulioko kusini mwa Yemen una umuhimu wa kijiografia, na mapambano kati ya jeshi la serikali na kundi la Houthi yanatokea mara kwa mara kaskazini na magharibi mwa mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako