• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza asema mazungumzo na chama cha Leba yamaanisha maafikiano ya pande zote

    (GMT+08:00) 2019-04-08 08:45:45

    Waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May amesema, mazungumzo na chama cha upinzani cha Leba ili kuvunja mvutano uliopo kuhusu Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya yanamaanisha maafikiano ya pande zote mbili.

    Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, waziri mkuu huyo ametetea uamuzi wa kufanya mazungumzo na chama cha Leba kuhusu Brexit, uamuzi ambao umezua hasira na lawama kutoka kwa wabunge wa chama chake.

    Wakati huohuo, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit Bw. Michel Barnier atakutana na waziri mkuu wa Ireland Bw. Leo Varadkar mjini Dublin baadaye leo. Viongozi hao wanatarajiwa kujadili hali ilivyo kuhusu Brexit, kabla ya mkutano wa Baraza la Ulaya utakaofanyika Brussels.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako