• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Safari ya mjumbe wa UM kwenda Yemen yaahirishwa

    (GMT+08:00) 2019-04-08 08:49:13

    Safari iliyopangwa ya Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen Martin Griffiths kwenda Sanaa, mji mkuu wa nchi hiyo unaodhibitiwa na waasi, imeahirishwa. Griffiths alitarajiwa kuwasili Sanaa Jumapili, kujadili utekelezaji wa Makubaliano ya Stockholm na waasi wa kundi la Houthi. Hata hivyo, ndege iliyowasili mapema siku hiyo mjini Sanaa ilibeba maofisa wengine wa Umoja wa Mataifa. Pande hasimu nchini Yemen zilifikia makubaliano ya amani mwezi Disemba mwaka jana mjini Stockholm kama ni hatua ya kwanza ya kuelekea kumalizia vita ya wenyewe kwa wenywe iliyodumu kwa miaka minne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako