• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Kenya Lionesses yazimwa Brazil, fainali kuzikutanisha Brazil na Scotland

    (GMT+08:00) 2019-04-08 08:55:22

    Matumaini ya Kenya kuwa na timu mbili kwenye michuano ya raga ya dunia yamezimwa baada ya timu ya taifa ya raga ya Kenya (Lionesses) kuzidiwa ujanja na Brazil katika nusu-fainali kwa alama 17-5 mjini Hong Kong mnamo Ijumaa katika mechi za kufuzu kushiriki raga ya dunia ya wanawake ya msimu 2019-2020.

    Lionesses, ambayo ilizimwa na Afrika Kusini katika nusu fainali ya mchujo wa mwaka 2018 mjini Hong Kong, iliingia mechi ya Brazil ikiwa na motisha ya kuipepeta Uganda 24-0, Hong Kong 36-5 na Papua New Guinea 20-10 katika mechi za kundi B na kuizaba Argentina 17-15 katika robo-fainali. Fainali ya michuano hiyo itazikutanisha timu za Brazil na Scotland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako