• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema Marekani italipizwa kisasi ikilichukulia Jeshi la Iran kuwa ni kundi la ugaidi

    (GMT+08:00) 2019-04-08 18:43:37

    Jeshi la ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limetoa taarifa likisema Marekani italipizwa kisasi kama ikilichukulia Jeshi hilo kuwa ni kundi la kigaidi.

    Baadhi ya vyombo vya habari kutoka nchi za magharibi siku hizi vimeripoti kuwa serikali ya Marekani inapanga kulichukulia Jeshi la ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran kuwa ni kundi la kigaidi. Kamanda Mkuu wa jeshi hilo Bw Mohammad-Ali Jafari ametoa taarifa akisema kama Marekani itachukua hatua hiyo na kutishia usalama wa Iran, basi jeshi hilo litailipiza kisasi. Amesisitiza kuwa kama Marekani inaamini kuwa jeshi hilo ni kundi la ugaidi, vikosi vya Marekani vitapoteza utulivu kwenye nchi za Asia Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako