• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NMB na NHC zatakiwa kushirikiana kutatua changamoto kwenye sekta ya nyumba Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-04-08 20:38:49

    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametoa wito kwa Benki ya NMB kuungana na Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), ili kusaidia utatuzi wa changamoto ya umiliki wa nyumba bora na za kisasa miongoni mwa Watanzania.

    Lukuvi alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa NMB Nyumba Day Expo 2019, maonyesho yanayolenga kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi na kutoa elimu na uelewa kwa wananchi juu ya mikopo ya nyumba na namna sahihi ya kumiliki nyumba bora.

    Lukuvi amesema kumekuwa na changamoto kubwa kwa Watanzania wa kada mbalimbali katika kumiliki viwanja, kupata hati za viwanja hivyo pamoja na vibali vya ujenzi na kwamba ushirikiano wa kikazi baina ya NMB na NHC, utasaidia kumaliza changamoto hiyo.

    Kupitia maonyesho hayo yanayofanyika jijini Arusha, Waziri Lukuvi alibainisha kuwa serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 421 kwa taasisi za fedha nchini humo kupitia Sheria ya Fedha za Mikopo ya Makazi ya Mwaka 2008, kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwezesha upatikanaji wa makazi ya kutosha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako