• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yatoa msaada wa chakula kwa waathiriwa wa njaa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-04-08 20:39:07

    Kampuni ya Chuanshan international, imetoa magunia 300 ya mahindi na katoni 20 za mafuta ya kupikia kwa waathiriwa wa njaa katika kaunti ya Baringo.

    Wakazi wa kijiji cha Katikit walionekana kufurahi baada ya kupokea bidhaa hizo na kutoa shukrani kwa kampuni hiyo ya China. Mkurugenzi wa kampuni ya Chuanshan, Han Ke alisema, wameamua kuchangaia juhudi za serikali ya Kenya kuokoa maisha ya wenyeji ambao wameathiriwa na ukame ambao ni mwingi hivi sasa katika maeneo mengi nchini Kenya.

    Kampuni hiyo ilikuwa ikigawa chakula kama sehemu ya jukumu lake la kusaidia jamii ya eneo hilo.

    Hata hivyo, kizaazaa kilizuka pale wakazi walipoanza kung'ang'ania magunia ya mahindi ambayo yalinuiwa kugawiwa vijiji saba ambapo wakazi wanakumbwa na uhaba wa chakula.

    Miongoni mwa vijiji hivyo ni Katikit, Chemusuk, Chemolingot, Kositei, Seretion, Kapturo na Chemisik.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako