• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuwa kitovu biashara ya chai Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-08 20:39:26
    Tanzania ina sifa duniani ya kuzalisha chai bora kutoka Nyanda za Juu Kusini, lakini kwa muda mrefu uzalishaji na uchakataji wa chai nchini humo umegubikwa na matatizo.

    Kutokana na hali hiyo, mwekezaji wa kampuni ya DL Group amejitosa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara na ulimaji wa chai Afrika. Chai ni kati ya mazao mkakati saba ya Tanzania.

    Mwenyekiti Mtendaji wa DL Group, Dk. David Langat, amesema jambo hili linawezekana kwa sababu wakulima wa Tanzania wana uzoefu wa kulima chai na serikali inathamini sekta binafsi na mapendekezo yake.

    Kampuni ya DL Group katika miaka mitatu ya nyuma imewekeza katika zao la chai nchini humo na kupambana na matatizo ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa wakulima.

    Langat alieleza kuwa kampuni yao imenunua mashamba na viwanda vilivyotelekezwa na wawekezaji na kulipa madeni ambayo wakulima wadogo walikuwa wakiwadai wawekezaji waliotoweka.

    DL Group imefufua mashamba na kupanda chai upya katika mikoa ya Njombe na Arusha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako