• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakamilisha ukaguzi wa Parachichi

    (GMT+08:00) 2019-04-08 20:39:43

    China imemaliza kukagua tunda la parachichi nchini Kenya baada ya kukamilisha ziara yao katika vituo mbali mbali vya kuandaa tunda hilo ikiwemo maabara na katika uwanja wa ndege. Wataalam wawili kutoa idara ya kukagua mazao nchini China walifika nchini Kenya wiki iliyopita na kumaliza ukaguzi wao leo jumatatu. Watalaam hao walikuwa wenyeji wa idara ya kukagua ubora wa mimea nchini Kenya Kephis. Watalaam hao walikuja kufuatia ombi la kukagua bidhaa hiyo kabla ya kupenya katika soko la China . Wataalm hao wanatarajiwa kuandika ripoti itakayoamua iwapo Kenya itasafirisha bidhaa hiyo nchini China au la. Hivi sasa wakulima wengi wana imani kuwa ripoti hiyo itakuwa nzuri kwao.Kama itawapa nafasi wakulima kusafirisha parachichi zao China basi itawaepusha na mawakala ambao wamekuwa wakiwapunja.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako