• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Rwanda apongeza juhudi za Macron kuchunguza nafasi iliyochukua Ufaransa katika mauaji ya kimbari

    (GMT+08:00) 2019-04-09 08:31:58

    Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema juhudi zilizofanywa na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ni "maendeleo makubwa" kuelekea kuchunguza nafasi ya Ufaransa katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994.

    Rais Macron wa Ufaransa ameteua wataalamu kuunda tume ya wanahistoria na watafiti kwa ajili ya kuchunguza nafasi ya Ufaransa katika mauaji ya kimbari ya Rwanda na kutoa ripoti kwa umma.

    Akiongea na wanahabari kufuatia kumbukizi ya miaka 25 ya mauaji hayo mjini Kigali, rais Kagame amesema hii ni hatua kubwa kwa jinsi kumbukumbu za historia zinavyoshughulikiwa, kwa kuwa zinabeba ukweli ambao watu wanaweza kufichua kuhusu nafasi iliyochukuliwa na Ufaransa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako