• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yapongeza makampuni ya China kwa juhudi zao katika miradi ya miundombinu

    (GMT+08:00) 2019-04-09 08:32:19

    Serikali ya Zambia imepongeza makampuni mawili ya ujenzi ya China kutokana na juhudi zilizofanya kwa ajili ya miradi mikubwa ya miundombinu mkoani Copperbelt.

    Katibu mkuu wa mkoa huo Bw. Bright Nundwe amepongeza kampuni ya AVIC International na kampuni ya CNCEC kutokana na maendeleo yaliyopatikana kwenye ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa na mradi wa maboresho ya huduma za utoaji maji.

    Bw. Nundwe amehimiza makandarasi wengine kuiga mfano wa makampuni hayo ya China katika kutelekeza miradi mbalimbali kwa ufanisi na ubora.

    Afisa huyo amesema mamlaka ya mkoa haitaruhusu ucheleweshaji wowote katika miradi mkoani humo, na pia ubora wa miradi unatakiwa kuhakikishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako