• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yaanzisha kiwanda cha kuchakata taka za plastiki nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-04-09 09:04:04

    Kampuni moja kutoka China jana imezindua kiwanda chenye thamani ya dola za kimarekani milioni 45 kinachochakata taka za plastiki mashariki mwa Kenya, ili kusaidia kuzuia uharibifu wa mazingira.

    Kampuni hiyo iitwayo Weeco inayotarajiwa kuchakata tani 2,000 za chupa za PET kila mwezi na kuzifanya ziwe vipande vidogo na nyuzi za plastiki, jana ilitangaza kuanzisha viwanda viwili nchini Kenya, ambavyo kimoja kitakuwa Athi River, mashariki mwa Kenya, na kingine mjini Mombasa.

    Kampuni ya Weeco pia imesaini makubaliano ya ushirikiano na kampuni ya PETCO Kenya, ambayo inasimamia mifuko ya PET baada ya kutumika nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako