Rais Vladimir Putin wa Russia na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamekubaliana kutekeleza makubaliano yao ya kusafirisha mifumo ya makombora ya Russia aina ya S-400 kwa Uturuki kama ilivyopangwa na pia nchi zao zitaanza uzalishaji wa vifaa vya kijeshi vyenye teknolojia ya hali ya juu. Uturuki ni nchi mwanachama wa kwanza wa Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO kununua mifumo ya makombora hayo, hatua iliyoamsha hasira ya Marekani. Mifumo hiyo ya ulinzi wa anga ni ya kisasa zaidi ya Russia na inaweza kubeba aina tatu za makombora.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |