• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi mpya wa China akabidhi hati za utambulisho kwa rais wa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-04-09 09:46:03

    Balozi mpya wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng jana amekabidhi hati za utambulisho kwa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, na pande hizo mbili zimefanya mazungumzo ya kirafiki.

    Rais Kenyatta amesema, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya Kenya na China umekuwa wa karibu zaidi, na ushirikiano kati nchi hizo mbili umepata mafanikio makubwa. Ameongeza kuwa Kenya inaishukuru serikali ya China na wananchi wake kwa kuiunga mkono kwa muda mrefu. Pia amesema Kenya inapenda kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta za biashara, kilimo na ujenzi wa miundombinu, ili kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya Kenya na China kuendelea zaidi.

    Bw. Wu amesema China inavichukulia pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kuwa ni fursa nzuri za kimaendeleo, na China inapenda kuimarisha ushirikiano kati yake na Kenya, ili kuwanufaisha wananchi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako