• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Shughuli za kutuma na kupokea pesa kwa zakua kwa asilimia 14 Januari

    (GMT+08:00) 2019-04-09 17:08:01
    Shughuli za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu nchini Kenya zimekua kwa asilimia 14 mwezi Januari 2019.

    Benki kuu ya Kenya imesema shilingi bilioni 368 zilitumwa kwa njia ya simu kwenye kipindi hicgo hasa kwa ulipaji wa karo na manunuzi.

    Takwimu za benki hiyo zinaonyesha kuwa kampuni za mawasiliano kama vile, Safaricom , Airtel na Telkom zilifanya matangazo mengi kwenye radio na runjinga na hivyo kuvutia wateja wanaotumia huduma za kifedha za simu.

    Kulingana na taakwimu za mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya, huduma ya Mpesa ya kampuni ya Safaricom inaongoza kwa mgao wa soko wa asilimia 80.8 Airtel asilimia 11.9 na Equitel asilimia 6.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako