• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini na China zafanya maonesho ya kazi ya pamoja kwa wanafunzi wa Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2019-04-09 17:26:19

    Maonesho ya kazi kwa ajili ya wanafunzi wa Afrika Kusini waliomaliza mazoezi yao ya kazi hapa China yamefanyika mjini Johannesburg ili kuwasaidia kupata ajira.

    Maonesho hayo yamewavutia wanafunzi 1000 wanaotafuta ajira kwenye makampuni maarufu ya China kama Shirika la ndege la China na Kampuni ya simu ya China Unicom, na makampuni mengine karibu arobaini yenye ofisi zao nchini Afrika Kusini.

    Maonesho hayo yameandaliwa kwa pamoja na wizara ya elimu ya juu na mafunzo, chama cha wafanyabiashara wa China na Afrika Kusini, na kituo cha utamaduni wa China na mabadilishano ya elimu ya kimataifa.

    Balozi wa China nchini Afrika Kusini Lin Songtian, amesema kuna haja kwa makampuni zaidi ya China kuwekeza nchini Afrika Kusini, na kuwa sehemu yake ya maendeleo ya kiuchumi. Pia amesema kwa sasa wanawahimiza wawekezaji wa China kuwekeza kwenye maendeleo endelevu na viwanda nchini Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako