• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari wasababisha vifo vya watu 5 wakiwemo askari watatu wa Marekani nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2019-04-09 18:58:18

    Jeshi la NATO nchini Afghanistan limetoa taarifa ikisema bomu lililotegwa katika gari limelipuka karibu na kituo cha jeshi la anga cha Bagram cha Marekani,na kusababisha vifo vya watu watano na wengine wanane kujeruhiwa.

    Mkuu wa idara ya polisi ya Bagram Bw. Naqib Kohistani, amesema, gari moja lililokuwa na mabomu lilipuka na mshambuliaji kufariki papo hapo. Askari waliouawa walikuwa kwenye doria, na walishambuliwa wakiwa njiani kurudi katika kituo hicho.

    Taarifa iliyotolewa na jeshi la NATO nchini humo, imesema mlipuko huo umesababisha vifo vya askari watatu wa Marekani na mkandarasi mmoja wa nchi hiyo, huku askari wengine tatu wa Marekani na raia watano wa huko wakijeruhiwa. Kundi la Taliban limetoa taarifa ikitangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako