• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taasisi ya utafiti wa mambo ya Afrika ya China yazinduliwa

    (GMT+08:00) 2019-04-09 18:59:23

    Mkutano wa uzinduzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Afrika ya China umefanyika leo hapa Beijing. Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Bw. Yang Jiechi, amehudhuria mkutano huo na kusoma barua ya pongezi ya rais Xi Jinping wa China.

    Bw. Yang amesema barua ya pongezi ya rais Xi imeonesha ufuatiliaji na uungaji mkono wake na upande wa China kwa uhusiano kati ya China na Afrika, na mawasiliano ya watu na utamaduni kati ya pande mbili, huku akisisitiza imani na nia ya pande mbili za China na Afrika kuendesha vizuri taasisi hiyo.

    Bw. Yang amesema, katika miaka ya hivi karibuni uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kwa pande zote kati ya China na Afrika unazidi kuimarika, pande mbili zinafanya juhudi kujenga ncha mpya za mawasiliano ya binadamu na utamaduni ukiwemo ushirikiano wa jumuiya za washauri bingwa, huku zikiendeleza mawasiliano ya utawala wa kiserikali na uzoefu wa maendeleo na kutafuta kwa pamoja mtindo mpya wa ushirikiano wa kunufaishana. Uzinduzi wa taasisi hiyo umeendana na sifa mpya na mwelekeo mpya wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, na kubeba matarajio mapya na matakwa ya kuimarisha ushirikiano wa taasisi za washauri bingwa za China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako