• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa bunge la Israel wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2019-04-09 19:27:21

    Israel leo imefanya uchaguzi wa 21 wa bunge, vyama na miungano wa vyama zaidi ya 40 vya siasa inagombea viti 120 vya bunge. Vituo zaidi ya elfu kumi vya kupigia kura vimefunguliwa kote nchini Israel, na wapiga kura wamejitokeza kwenye vituo hivyo ambavyo vitafungwa saa nne usiku.

    Kwa mujibu wa takwimu za Tume kuu ya uchaguzi, kuna wapiga kura milioni 6.34 nchini Israel wanaostahili kupiga kura, na kiwango cha upigaji kura kinatarajiwa kufikia asilimia 70.

    Waziri mkuu wa Israel ambaye pia ni kiongozi wa Likud Bw. Benjamin Netanyahu amepiga kura huko Jerusalem. Kiongozi wa Chama cha Bluu na Nyeupe Bw. Benny Gantz amepiga kura katika mji wa Rosh Ha'ayin, katikati ya Israel.

    Kwa mujibu wa kura za maoni za hivi karibuni, Chama cha Bluu na na Nyeupe na cha Likud vinaongoza, huku Chama cha Leba na muungano wa vyama vya Kiarabu vikifuata.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako