• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka nchi kubwa za kigeni zichangie amani na utulivu kwenye Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2019-04-09 19:34:48

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema China inataka nchi kusika haswa nchi kubwa zichangie katika kuhimiza amani na utulivu kwenye eneo la Mashariki ya Kati, na kuepuka kuchukua hatua inayochochea hali ya wasiwasi kwenye kanda hiyo.

    Rais Donald Trump wa Marekani jana ametoa taarifa akitangaza rasmi kuwa serikali ya nchi hiyo inapanga kulitaja Jeshi la ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kuwa ni kundi la kigaidi. Baraza kuu la usalama wa Iran limetoa taarifa kuwa hatua hiyo ya Marekani ni tishio kubwa kwa utulivu na amani ya kikanda na kimataifa, Iran italipiza kisasi kwa Marekani kama ikifanya hivyo.

    Kuhusina na suala hilo, Bw Lu Kang amesema China inapendekeza siku zote kuwa inapaswa kufuata kanuni za kimsingi chini ya Katiba ya Umoja wa Mataifa katika kutatua uhusiano kati ya nchi, ili kuepusha hatua itakayochochea hali ya wasiwasi kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako