• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yajiandaa kuboresha fursa za mapinduzi ya nne ya kiviwanda

    (GMT+08:00) 2019-04-10 08:40:21

    Uganda imeunda kikosi kazi cha taifa kitakachoishauri serikali juu ya maendeleo ya ndani ya teknolojia kutokana na mapinduzi ya nne ya kiviwanda ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi hiyo.

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezindua kikosi kazi hicho mjini Kampala, na kukitaka kulenga zaidi kwenye teknolojia ambazo zinashughulikia masuala ya ndani kama vile kuongeza uzalishaji wa kilimo, ambacho ni kitega uchumi kwa wananchi wengi wa nchi hiyo.

    Kikosi kazi hicho chenye watu 23 wakiwemo wahandisi, wanasayansi na wasomi, pia kitaishauri serikali kuhusu teknolojia zisizofaa ambazo zinapaswa kuepukwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako