• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania awaonya maofisa wanaowatisha wawekezaji

    (GMT+08:00) 2019-04-10 08:41:06

    Rais wa Tanzania John Magufuli amewaonya maofisa wanaowatisha wawekezaji wanaotaka kufanya biashara nchini humo, na kusema atawashughulikia ipasavyo.

    Rais Magufuli amesema hayo baada ya kuzindua kiwanda cha kuchakata majani ya chai chenye thamani ya Euro milioni 19 kinachomilikiwa na Unilever mkoani Njombe, kusini mwa Tanzania. Amesema maofisa wanaoshughulika na sekta mbalimbali ikiwemo mazingira, usalama sehemu za kazi na uhamiaji wanapaswa kutowatisha wawekezaji ambao wako tayari kufanya biashara nchini humo.

    Wakati huohuo, mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) nchini Tanzania Dr. Hassan Abbas amesema, rais wa Tanzania John Magufuli ametimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni ya uchaguzi wa rais. Amesema athari za mageuzi yaliyopendekezwa na rais Magufuli pamoja na serikali yake zinaweza kuonekana katika sekta zote ikiwemo kupambana na ufisadi na kuondoa umasikini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako