• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Umoja wa Ulaya zatoa taarifa ya pamoja kuhusu mkutano wa 21 wa viongozi wa pande mbili

    (GMT+08:00) 2019-04-10 08:59:59

    China na Umoja wa Ulaya zimetoa taarifa ya pamoja, zikisisitiza kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande hizo mbili na kuahidi kulinda utaratibu wa pande nyingi na kupinga sera za kujilinda kibiashara.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk na mwenyekiti wa kamisheni ya Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker walikutana jana kwenye mkutano wa 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya na kutoa taarifa hiyo ya pamoja.

    Pande hizo mbili zimesisitiza heshima yao kwa sheria ya kimataifa na kanuni za kimsingi za mahusiano ya kimataifa, ambazo Umoja wa Mataifa ni kiini chake.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao wameahidi kulinda katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa, na nguzo zote tatu za mfumo wa Umoja wa Mataifa, ambazo ni amani na usalama, maendeleo na haki za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako