• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza ajiandaa kushinda kuahirisha Brexit

    (GMT+08:00) 2019-04-10 09:06:56

    Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amerudi London baada ya jitihada zake za siku moja za kutafuta fursa ya kuahirisha nchi yake kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya. May alifanya mazungumzo na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa mjini Paris, na mjini London timu ya mawaziri wake walifanya mazungumzo na waziri kivuli wa chama cha Leba, John McDonnell na mawaziri wengine kivuli kutoka chama kikuu cha upinzani. Vyombo vya habari mjini London vimeripoti kuwa, rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk amewaandikia barua viongozi 27 wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, kuwataka waipe Uingereza muda wa mwaka mmoja wa mchakato wa Kifungu cha 50, hatua ambayo itairuhusu Uingereza kujitoa wakati wowote ndani ya kipindi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako