• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi ya Mabingwa Ulaya- Liverpool yaichezesha mchakamchaka Porto, Spurs yaipiga Man City

  (GMT+08:00) 2019-04-10 09:43:05

  Ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali imerejea jana kwa michezo miwili kupigwa, Liverpool ya Uingereza imekutana na FC Porto na kuendeleza ubabe uliofanya msimu uliopita kwa kuibamiza Porto goli 2-0.

  Mchezo mwingine ulikuwa baina ya Tottenham Hotspur ilipoikaribisha Manchester City katika uwanja wao mpya wenye uwezo wa kubeba mashabiki 62,000 uliopo kaskazini mwa jiji la London.

  Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi kikipulizwa, Tottenham waliibuka na ushindi wa goli 1-0.

  Ligi hiyo inaendelea leo kwa mechi kati ya Barcelona itakapovaana na Manchester United uwanja wa Old Trafford, huku Ajax itakutana na bibi kizee wa Turin Juventus.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako