• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Sudan waambiwa wasivamie maandamano ya amani

    (GMT+08:00) 2019-04-10 10:14:46

    Jeshi la Polisi la Sudan limevitaka vikosi vyote vya polisi vya nchi hiyo kutoshambulia raia au maandamano yanayofanywa kwa amani.

    Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo imesema, polisi pia wametakiwa kutekeleza majukumu yao ya kulinda maisha na mali za raia, kuzuia uhalifu, na kushughulikia mawasiliano ya barabara na usalama wa umma.

    Aidha mamlaka hiyo imeonya raia wa nchi hiyo wasifanye uharibifu, na kuahidi utayari wa kupambana na uhalifu.

    Habari nyingine zinasema, Marekani, Uingereza na Norway zimehimiza serikali ya Sudan kujibu matakwa ya waandamanaji ya kutaka kuwe na mpito wa kisiasa unaofuata sheria.

    Sudan imeshuhudia maandamano makubwa kote nchini humo tangu Disemba 19 mwaka jana, kutokana na hali mbaya ya uchumi na mfumuko wa bei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako