• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini kurekebisha sheria nne za usalama ili kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2019-04-10 10:16:13

    Kamati ya Marekebisho ya Katiba nchini Sudan Kusini imewasilisha miswada ya marekebisho ya sheria nne za usalama kwa wizara ya mambo ya sheria na katiba, ili kuhimiza utekelezaji mzuri wa makubaliano ya amani.

    Sheria hizo ni pamoja na sheria ya ukombozi wa watu wa Sudan, sheria ya huduma za polisi, sheria ya huduma za magereza na sheria ya huduma za wanyamapori.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Gichira Kibara amesema, nchi hiyo inafanya marekebisho makubwa ya sekta ya usalama, na kukumbusha kuwa kuwasilishwa kwa miswada hiyo ni msingi wa kutekeleza makubaliano ya amani.

    Naye waziri wa mambo ya sheria na katiba ya nchi hiyo Bw. Paulino Wanawilla Unango amesema, kazi yake ni kuharakisha miswada hiyo kupita kwenye utaratibu wa kisheria, ili ipitishwe mapema na bunge na kuwa sheria rasmi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako