• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waafrika wafurahia uzinduzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Afrika ya China

    (GMT+08:00) 2019-04-10 10:18:15

    Mkutano wa uzinduzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Afrika ya China ulifanyika jana mjini Beijing, na rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongeza kwa mkutano huo.

    Watu kutoka nyanja mbalimbali wa Afrika wamesema taasisi hiyo itachangia busara na mchango zaidi kwa ajili ya maendeleo ya uhusiao kati ya pande hizo mbili.

    Mtaalamu wa uhusiano kati ya Afrika na China kutoka Kenya Bw. Edhurley Cavens ameeleza matumaini yake kuwa taasisi hiyo itakuwa daraja la kuhimiza mazungumzo na ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Katibu wa ngazi ya juu wa rais wa Uganda anayeshughulikia mambo ya habari Bw. Don Vanyama amesema taasisi hiyo itafanya kazi kubwa katika kukuza uhusiano kati ya China na Afrika na urafiki kati ya pande hizo mbili.

    Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Walter Sisulu cha Afrika Kusini Bw. Eric Manguni amesema, kuanzishwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Afrika ni hatua muhimu ya China katika kukuza mawasiliano ya watu na utamaduni kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako