• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia yafanya majaribio ya mbinu za uhifadhi wa misitu kuhimiza kuzoea hali mpya

    (GMT+08:00) 2019-04-10 17:07:23

    Ofisa wa serikali wa Namibia amesema wizara ya kilimo, maji na misitu ya nchi hiyo na Chuo Kikuu cha Namibia wanaendesha majaribio ya mbinu za uhifadhi wa misitu ili kuboresha mazingira na kilimo endelevu.

    Majaribio hayo yanafanyika kwenye kituo cha maendeleo ya umwagiliaji cha Mashare, kaskazini mashariki mwa Namibia.

    Ofisa wa idara ya maendeleo ya kilimo na uhandisi ya wizara ya kilimo ya Namibia Bw. Berefine Antindi, amesema mradi huo ni sehemu ya mpango wa uhifadhi wa kilimo wa taifa, na ulianzishwa kwenye mpango wa tano wa maendeleo ya taifa, ukiwalenga asilimia 50 ya wakulima kabla ya mwaka 2022.

    Namibia imekuwa ikisumbuliwa na ukame wa mara kwa mara unaoathiri asilimia 60 ya kaya za nchi hiyo zinazotegemea kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako