• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ahimiza kuwekeza zaidi katika elimu bora

    (GMT+08:00) 2019-04-10 19:30:58

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu bora na kazi yenye heshima kwa vijana.

    Bw. Guterres amesema hayo katika kikao cha ufungaji wa kongamano la nane la vijana la baraza la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, huku akionya kuwa hivi sasa vijana wanakabiliwa na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira na hisia ya kawaida ya kunyimwa kwa haki halali.

    Kwa mujibu wa katibu mkuu, vijana milioni 64 wanakosa ajira na wafanyakazi vijana wapatao milioni 145 wanaishi katika hali ya umaskini, huku vijana milioni 617 kote duniani wakikosa ujuzi wa kimsingi wa kuhesabu, kusoma na kuandika.

    Pia amesema wasichana huwa wanapuuzwa kutoka kwenye afya mpaka elimu, kutoka upatikanaji wa nafasi za ajira hadi upatikanaji wa mitaji, huku akiongeza kuwa katika baadhi ya sehemu, kiwango cha ukosefu wa ajira cha wanawake ni maradufu ya kiwango hicho kwa wanaume.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako