• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Teknolojia kutumika ili kukabili bidhaa gushi

    (GMT+08:00) 2019-04-10 19:45:37
    Halmashauri ya ubora wa bidhaa nchini Rwanda imesema hivi karibuni itazindua nembo mpya ambayo itatumika kuidhinisha bidhaa zote ambazo zimetimiza viwango.

    Afisa wa halmashauri hiyo Anicet Muriro, amesema pia mbali na nembo hiyo mpya kwa jina S-mark, serikali itatumia teknolojia ili kukamata bidhaa gushi.

    Amesema hatua hiyo itasaidia bidhaa za Rwanda kwenye soko la ndani na pia lile la kimataifa.

    Rwanda imekuwa na kampeni ya tangu mwaka 2015 ya kuhimiza utengenezaji wa ndani wa bidhaa iki kukuza viwanda.

    Tangu mwaka huo mauzo ya nje yameongezeka kwa asilimia 69 na kuiletea nchi hiyo dola milioni 944.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako