• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: TBS yatoa elimu wilayani

    (GMT+08:00) 2019-04-10 19:46:14
    Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemaliza kampeni yake ya kutoa elimu kwa umma katika wilaya kadhaa zikiwemo Nachingwea, Kilwa, Songea, Bukoba, Kahama, Tarime, Nyamagana, Korogwe, Kilombero na Kisarawe Juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo.

    Kampeni hiyo ya elimu kwa umma imefanyika katika maeneo mbalimbali zikiwamo shule za msingi na sekondari, masoko, stendi, minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi walijitokeza kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo ubora wa bidhaa.

    Ofisa Masoko Mwandamizi, Gladness Kaseka, aliwakumbusha wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ni ya Taifa kwa ujumla.

    Aliwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwapo wa bidhaa hafifu katika soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako