• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Vijiji zaidi ya 9,000 kupata umeme

    (GMT+08:00) 2019-04-10 19:46:32
    Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaondoa hofu wabunge kuhusu usambazaji wa umeme unaofanywa na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) ambapo hadi kufikia Julai mwaka 2020 vijiji 9,055 vitakuwa na umeme.

    Ameyasema hayo wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu na Mfuko wa Bunge mwaka 2019/2020

    Amesema tangu julai Mosi, 2016 hadi 30 Machi mwaka huu vijiji 1,969 vilipata umeme na ukichanganya na vijiji ambavyo vilikuwa vimeshapatiwa umeme kabla ya Juni mwaka 2016 inakuwa jumla ya 6,365 kati ya vijiji 12,268.

    Amesema hiyo ni sawa na asilimia 52 ya vijiji vyote kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako