• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kampuni ya chai DL Group yajenga ghala

    (GMT+08:00) 2019-04-10 19:47:17
    Kampuni ya DL Group ambayo kwa miaka mitatu iliyopita imejikita katika kuwekeza katika zao la chai nchini, imejenga ghala kubwa litakalowapunguzia wazalishaji gharama ya asilimia 50 ya usafirishaji na kujenga mazingira ya usimamizi mzuri ya kuwapo mnada wa kikanda wa chai nchini Tanzania.

    Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Dk. David Langat, alisema jijini Nairobi, Kenya, kuwa chai ni zao mkakati katika shughuli za kampuni yao na kwamba kampuni hiyo imedhamiria kushirikiana kwa karibu na serikali na wakulima kukuza ulimaji na biashara ya chai nchini Tanzania.

    Alisema nia ya kampuni yao ni kuhakikisha mnada wa chai kutoka Tanzania, Rwanda, Burundi na Malawi unafanyika Dar es Salaam na chai hiyo inasafirishwa nje kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako