• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na mwenzake wa Croatia

    (GMT+08:00) 2019-04-10 21:02:40

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo huko Zagreb amekutana na mwenzake wa Croatia Bw. Andrej Plenkovic.

    Bw. Li alipokutana na Bw. Plenkovic amesema, China inapenda kuzidisha kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mkakati wa maendeleo ya Croatia, kuzidishathamani ya biashara za pande mbili, kuinua kiwango cha uwekezaji kwa upande mwingine, na kuongeza kuagiza bidhaa zenye sifa ya Croatia zinazokidhi mahitaji ya soko la China.

    Bw. Plenkovic amesema, Croatia inapenda kuimarisha ufahamu wa historia na utamaduni wa China, kunufaishwa na fursa ya maendeleo ya China, kuunga mkono ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili. Bw. Li pia amekutana na spika wa bunge la nchi hiyo Bw. Gordan Jandrokovic.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako