• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu ya soka ya wanawake- Thika Queens njia panda

  (GMT+08:00) 2019-04-11 08:47:20
  Mabingwa wa zamani katika ligi kuu ya soka la wanawake ya Kenya (KWPL), Thika Queens wameona giza baada ya kupigwa kwa mabao 2-0 na Oserian Ladies kwenye mechi iliyochezewa uwanjani Oserian mjini humo.

  Mabao ya Oserian yalipachikwa kimiani na Rebecca Akinyi na Margaret Omweri. Matokeo mengine, GASPO Women wameichapa Makolanders bao 3-2, Wadadia LG imelazimishwa sare ya 1-1 na Kayole Starlets, nayo Trans-Nzoia Falcons imeendelea kutembeza kipigo na kuvuna alama tatu muhimu baada ya kuichapa Mathare United ya wanawake 6-2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako