• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Robo fainali ya Ligi ya Ulaya kupigwa leo-Arsenal atakuwa nyumbani huku Chelsea yupo ugenini

  (GMT+08:00) 2019-04-11 08:49:54
  Baada ya kuangukia pua kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi iliyopita, Arsenal wanatarajia kufanya vizuri leo watakapocheza mchezo wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya Ulaya.

  Washika bunduki hao watakuwa nyumbani kuikabili Napoli ukiwa ni mchezo muhimu sana kwa Arsenal kupata matokeo mazuri.

  Chelsea wao watakuwa wageni wa Slavia Prague kwenye mchezo ambao watahitajika kushinda licha ya kuwa katika kiwango kizuri katika michuano hii. Slavia licha ya kutopewa nafasi sana ya kushinda, lakini wameonyesha wana kila uwezo wa kufanya vizuri.

  Michezo mingine ni kati ya Benfica itavaana na Eintracht Frankfurt, nao Valencia watakutana na Villareal.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako