• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Picha ya kwanza ya Shimo Jeusi (Black Hole) yapatikana

    (GMT+08:00) 2019-04-11 08:53:59

    Wanaanga wametangaza jana kuwa wamefanikiwa kuchukua picha ya kwanza ya Shimo Jeusi (Black Hole), inayotoa ushahidi wa kwanza unaoonekana wa Shimo hilo na kivuli chake.

    Darubini kubwa inayoitwa Event Horizon Telescope EHT inayounganisha darubini nane duniani imefanikiwa kupiga picha Shimo Jeusi kwenye kiini cha galaxy kubwa ya M87, iliyoko umbali wa Miaka ya Nuru milioni 55 kutoka sayari ya Dunia na yenye uzito wa mara bilioni 6.5 kuliko Jua.

    Mkurugenzi wa mradi wa EHT Bw. Sheperd Doeleman ameitaja picha hiyo kuwa ni "ugunduzi wa kushangaza" na "muujiza", na kuwa matokeo hayo yametoa mbinu mpya kwa wanasayansi kutafiti Shimo Jeusi angani linalotabiriwa na nadharia ya General Relativity iliyobuniwa na Albert Einstein.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako