• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shelter Afrique yashirikiana na China katika kutatua msukosuko wa nyumba barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-11 08:54:57

    Taasisi ya huduma za kifedha kwa mali zisizohamishika ya Afrika inatafuta kushirikiana na China kwa ajili ya kumaliza msukosuko wa nyumba barani Afrika.

    Akiongea kando ya Mkutano wa sita wa mwaka wa Uwekezaji wa Mali katika Afrika Mashariki, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shelter Afrique Bw. Andrew Chimphondah ameliambia Shirika la habari la Xinhua mjini Nairobi kuwa, serikali za nchi 44 za Afrika zinamiliki asilimia 78 ya hisa za ngazi A za taasisi hiyo, huku Benki ya Maendeleo ya Afrika na Kampuni ya African Reinsurance zikimiliki asilimia 22 za hisa za ngazi B.

    Bw. Chimphondah amesema Shelter Afrique imezindua hisa mpya ya ngazi C ambayo wanatumai kuziuza kwa taasisi za huduma za kifedha za China, ili kuziwezesha kusaidia katika ujenzi wa nyumba zenye bei nafuu barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako