• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kushiriki kwenye maonesho ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-11 09:16:37

    Mamlaka ya maendeleo ya biashara ya Tanzania (TanTrade) jana imezihimiza kampuni za nchi hiyo kutumia fursa nzuri zitakazotolewa na maonesho ya biashara yatakayofanyika mwezi Juni mwaka huu nchini China.

    Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Mamlaka hiyo imesema, Tanzania itashiriki kwenye maonesho ya kwanza ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yatakayofanyika huko Changsha, mkoa wa Hunan nchini China, yenye kauli mbiu ya "ushirikiano wa kunufaishana unaoimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika".

    Taarifa pia imesema, maonesho hayo yatafuatilia biashara, uwekezaji, mambo ya kifedha, kilimo, madini, nishati, utalii na miundombinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako