• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya usalama nchini Sudan yaunga mkono maandamano ya Amani na kuonya dhidi ya vurugu

    (GMT+08:00) 2019-04-11 09:16:55

    Idara ya usalama na nchini Sudan (NISS) imetangaza kuunga mkono haki ya maandamano ya Amani, lakini imeonya dhidi ya vurugu.

    Katika taarifa yake, Idara hiyo imesema haki ya maandamano ya Amani imehakikishwa na katiba ya nchi hiyo, na kuonya dhidi ya majaribio yoyote ya kuanzisha vurugu na uharibifu wa usalama nchini humo.

    Jumamosi wiki iliyopita, mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ulishuhudia maandamano yaliyotokana na hali mbaya ya kiuchumi na kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu za matumizi.

    Wakati huohuo, mamlaka ya usalama mjini humo iliamua kufuta maandamano yaliyoandaliwa kufanyika leo ili kumuunga mkono rais Omar al-Bashir wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako