• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Croatia kuimarisha ushirikiano wa utamaduni na utalii

    (GMT+08:00) 2019-04-11 09:17:18

    Waziri mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic na waziri mkuu wa China Li Keqiang wamesema nchi hizo mbili zitaimarisha ushirikiano wa utamaduni na utalii.

    Mawaziri hao wamesema hayo walipozungumza katika hafla ya Mwaka wa Utalii kati ya China na Croatia iliyofanyika jana. Waziri mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic amesema, watu wa nchi yake wanavutiwa sana na utamaduni wa China, na kwamba mwaka huo wa utalii utaimarisha zaidi urafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Naye waziri mkuu wa China Li Keqiang ambaye yuko ziarani nchini Croatia, amesema serikali ya China inaunga mkono juhudi za nchi hizo mbili katika kupanua ushirikiano wa utalii, na kuongeza kuwa Wachina 250,000 walitembelea Croatia mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako