• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe atoa wito wa misaada zaidi kwa watu walioathiriwa na kimbunga Idai

    (GMT+08:00) 2019-04-11 09:28:55

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana katika ikulu ya nchi hiyo amekutana na wafanyabiashara na wadau wengine, na kuwataka watoe misaada zaidi kwa ukarabati wa miundombinu kutokana na uharibifu uliosababishwa na kimbunga Idai kilichotokea Machi.

    Kampuni kadhaa zimeahidi kuchangia ukarabati wa shule na miundombinu iliyoharibiwa.

    Kabla ya mkutano huo, serikali ya Zimbabwe imesema dola za kimarekani milioni 612 zinahitajika kwa ajili ya chakula, malazi na ukarabati wa miundombinu.

    Hadi sasa idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga hicho imefikia 344, na huenda ikaongezeka zaidi baada ya miili mingine kupatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako