• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatangaza kupiga marufuku mifuko ya plastiki inayotumika mara moja

    (GMT+08:00) 2019-04-11 09:29:18

    Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa ametangaza kupiga marufuku mifuko yote ya plastiki inayotumika mara moja tu kuanzia tarehe mosi Juni, mwaka huu.

    Bw. Majaliwa ametoa tangazo hilo bungeni akisema, marufuku hiyo itahusisha uzalishaji, uagizaji kutoka nje, mauzo na matumizi ya mifuko ya plastiki inayotumika mara moja na kutupwa, ili kupunguza uchafuzi.

    Amesema sheria husika iko tayari, na itatangazwa rasmi na serikali.

    Awali, Kenya ilitoa marufuku kali zaidi duniani dhidi ya matumizi ya mifuko ya plastiki, na yeyote anayekiuka marufuku hiyo atapewa adhabu ya kifungo cha miaka minne, au kutozwa faini ya dola za kimarekani elfu 40.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako