• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CPI ya China kwa mwezi Machi iliongezeka kwa asilimia 2.3

    (GMT+08:00) 2019-04-11 17:31:51

    Taasisi ya takwimu ya China NBS, imesema faharisi ya bei za walaji ya China yaani CPI, inayopima mfumuko wa bei, iliongezeka kwa asilimia 2.3 katika mwezi Machi, likiwa ni ongezeko la asilimia 1.5 kuliko mwezi Februari.

    Bei za vyakula zilipanda kwa asilimia 4.1, likiwa ni ongezeko la asilimia 0.7 ikilinganishwa na mwezi Februari.

    Kutokana na mavuno ya kidogo ya mboga katika majira ya spring na mvua yenye baridi, bei za mbogamboga zilipanda kwa asilimia 16.2, na kuongeza kiwango hicho kwa asilimia 0.42.

    Bidhaa zisizo chakula ziliongezeka bei kwa asilimia 1.87, ikiwa ni asilimia 0.1 kuliko mwezi Februari. Na bei za petrol na dizeli zilipanda kwa asilimia 3.6 na 4 mtawalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako