• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF, Benki ya Dunia na WTO zaonya kuwa kupunga kwa kasi ya biashara ya dunia kutakwamisha upunguzaji wa umaskini

    (GMT+08:00) 2019-04-11 18:35:15

    Wakurugenzi kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Benki ya Dunia na Shirika la Biashara Duniani WTO jana wametahadharisha kuwa kupunga kwa kasi ya biashara ya dunia kunaweza kuathiri ubora wa maisha ya watu maskini na kukwamisha upunguzaji wa umaskini.

    Mkurugenzi mkuu wa IMF Bibi Christine Lagarde amesema biashara inatoa mchango mkubwa katika kupunguza umaskini, kwa kuwa biashara ya dunia inapunguza gharama ya mahitaji ya maisha.

    Ofisa mkuu mtendaji wa Benki ya Dunia Bibi Kristalina Georgieva amesema biashara inasaidia ukuaji wa uchumi, kuongeza nafasi za ajira pamoja na kupunguza umaskini, lakini kupungua kwa kasi ya biashara ya dunia kutakwamisha kazi ya kupunguza umaskini.

    Mkurugenzi mkuu wa WTO Bw Roberto Azevedo amesema kama biashara ya dunia itasimama, watu maskini wataathiriwa vibaya na kupunguza uwezo wao wa manunuzi. Amesema WTO inadhamiria kuhimiza biashara duniani ili kuhakikisha watu wote duniani wananufaishwa na biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako