• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Uganda Airlines kuanza kurusha ndege zake mwezi Agosti

    (GMT+08:00) 2019-04-11 18:49:29
    Shirika la ndege la Uganda litachukua hadi miezi mitatu kabla kuanza safari za ndege za biashara.

    Haya ni kulingana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Uganda ,Monica Azuba Ntege.

    Shirika hilo la ndege ambalo linatarajiwa kuleta ndege mbili kabla mwezi Aprili na Julai kuisha,Azuba alisema ndege hizo zitafanya maonyesho kwa kuruka nchi jirani pamoja na kukamilisha michakato mingine kama vibali.

    Akizungumza jijini Kampala jana,Azuba aliwaambia waandishi wa habari kuwa ndege hizo zitawasili tarehe 23 mwezi huu wa Aprili.

    Aidha Bi Azuba alisema kuwa ndege hizo zitawasili kwa awamu huku nyingine zikitarajiwa kuwasili mwezi Julai na Septemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako