• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazalishaji sekta ya usindikaji vyakula wapewa mafunzo

    (GMT+08:00) 2019-04-11 18:49:52

    Wazalishaji katika sekta ya usindikaji wa vyakula na sekta nyingine nchini Tanzania wameanza kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wa kati katika matumizi sahihi ya kemikali za viwandani ili kuwarahisishia kufikia ubora wa bidhaa wanazozizalisha.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo ( Sido) Mkoa wa Dodoma, Sempeho Manongi alisema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwapatia ujuzi sahihi wa awali wa matumizi ya kemikali ili kulinda watumiaji wa bidhaa.

    Manongi alisema matumizi salama na bora ya kemikali yanaendana na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya tano ya ujenzi wa Tanzania ya Viwanda katika kufikia uchumi wa kati.

    Manongi alisema Jiji la Dodoma pekee kuna wajasiliamali zaidi ya 2,000 wanaozalisha bidhaa za aina mbalimbali.

    Kwa upande wake, Meneja wa TFDA Kanda ya Kati Dk. Engelbert Mbekenga alisema watafundisha namna ya usindikaji salama wa vyakula na matumizi sahihi ya kemikali katika utengenezaji bidhaa mbalimbali, jinsi ya kufungasha na kuweka lebo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako