• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wakubali kurefusha muda wa Brexit hadi mwisho wa Oktoba

    (GMT+08:00) 2019-04-11 18:54:28

    Baada ya majadiliano ya saa kadhaa, mkuu wa baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk amefanya mkutano wa waandishi wa habari na kusema nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubali kurefusha muda wa Brexit hadi tarehe 31 mwezi Oktoba, hivyo Uingereza itakuwa na miezi sita za ziada za kupata ufumbuzi mzuri kabisa wa kutatua suala hilo.

    Baada ya hayo, baraza la Ulaya limetoa taarifa kuwa kabla ya tarehe hiyo, Uingereza haiwezi kufanya vitendo vitakavyovuruga maslahi ya Umoja wa Ulaya, na kama haitafikia makubaliano ya Brexit mpaka tarehe 22 mwezi Mei, inatakiwa kushiriki uchaguzi wa bunge la Ulaya kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Ulaya. Na baraza hilo litaendelea kushughulikia mambo ya Brexit na kuchagua maendeleo kwenye mkutano wa mwezi Juni.

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May anadhani Uingereza inatakiwa kujitoa Umoja wa Ulaya kwa makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako