• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Bei ya unga mahindi yaongezeka

    (GMT+08:00) 2019-04-11 19:04:18

    Kampuni za kusaga unga wa mahindi nchini Kenya zimeongeza maradufu bei ya bidhaa hiyo kutokana na uhaba wa mahindi,hatua ambayo huenda ikaongeza shinikizo kwenye mfumuko na kuathiri bajeti za nyumba nyingi.

    Mfuko wa kilo mbili wa unga wa mahindi wa Jogoo unauzwa Sh110 kutoka S102 siku mbili zilizopita.

    Unga huo wa Jogoo uliuzwa Sh90 ijumaa iliyopita kabla ya bei kuongezeka hadi Sh101 jumatatu,kumaanisha kuwa bei ya bidhaa hiyo imeongezeka kwa Sh19 au asilimia 21 ndani ya wiki moja.

    Hata hivyo serikali imewalaumu wafanyabiashara biashara kwa kuhodhi mahindi ili kuongeza bei,ikisisitiza kuwa nchi ina mahindi ya kutosha baada ya mavuno ,mazuri mwaka jana.

    Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri alisema Kenya ilipata mavuno ya amgunia milioni 40.9 ya mahindi mwaka jana,yanayoashiria ongezeko la asilimia 20 lililotarajiwa kusababisha bei ya unga wa mahindi kushuka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako